AINA ZA KEKI
kuna aina nyingi sana za keki. kila mpishi atakua ana aina zake kulingana na vitu alivyotumia katika mapishi yake.
Tofauti kubwa sana kwenye aina hizi za keki ni viamba upishi vilivyotumika, japo lengo ni moja tu la kupika keki yenye ladha iliyotarajiwa. kuna aina kuu saba za keki, nazo ni;
Aina za keki.
- keki ya chocolate
- keki ya vanilla
- keki ya mafuta
- keki ya limao
- keki ya karoti
- keki ya nazi
- keki ya red velvet
- keki ya chungwa
Hadi sasa zipo aina nyingi, na kila siku wapishi wa keki wanabuni aina mpya za keki.
Aina zote hizi za keki zinaweza tumika katika matukio mbalimbali kama vile:
- Harusi
- siku ya kuzaliwa (Birthday)
- kumbukizi ya harusi (wedding anniversary).
Unatakiwa kuzingatia ukubwa wa tukio, wingi wa watu watakaohudhuria tukio, jinsia ya mwenye tukio pamoja na rika.
Mambo yote haya nayo yanachangia katika kuleta aina tofauti za keki.
Ndio maana kuna keki za watoto wa kiume na keki za watu wa kike, hii yote ni kunogesha tukio kwa keki husika kwa mtu husika.
Mapambo yanachangia kuleta utofauti wa keki, na sasa tuna aina za keki kulingano na aina ya mapambo yalotumika kaama vile:
- Keki plain(isiyo na mapambo)
Aina hii ya keki, hua haipambwi. Ikishaiva tu bas inapoa na kua tayari kwa kuliwa.
Mara nyingi keki hii hutumika kwa chai, kahawa na juice au soda.
keki plain hua haihitaji tukio, huliwa tu kama vitafunwa vingine.
Na kwa wale ambao hawapend sukari nyingi, keki plain kwao ndo inakua nzuri zaidi.
kwani mara nyingi mapambo ya keki yanahusisha sukari nyingi sana.
- Keki ya fondant
keki ya fondant, hua inapambwa kwa kutumia fondant. Fondant inauzwa kwenye masupermarket au unaweza ukaitenegeneza mwenyewe nyumbani na ukaitumia kupambia keki yako.
Fondant inakua ni donge ambalo unalisukuma kama chapati na kufunika kwenye keki.
Fondant ni nzuri sana kwa ajili ya kutenegezea maua ya kwenye keki au muundo wa kitu chochote kwa ajili ya kunogesha keki yako.
- Keki ya Icing
Keki ya ising ndio maarufu zaidi. mchanganyiko wake hauna mambo mengi na ndio mara nyingi hutumika kwatika kupikia keki zenye mapambo ya kawaida. Ubunifu ndo hua unatofautisha lakini keki za ising zote zinapambwa kwa kitu kimoja tu "icing sugar"
- Keki ya kioo(Mirror gaze)
Keki hii inamwamwigia mchanganyiko wa maziwa, gelatin na vitu vingine na kuleta muonekano wa mngáo kama kioo. Mara nyingi keki hiz hua hazina mambo mengi zaidi ya huo mchanganyiko.
Ubunifu katika mapish na mapambo ndo yamezaliwa aina zote hiz za keki, na kila aina ya keki ina uzuri wake na utamu wake. Na uzuri ni kwamba kila mtu anacho anachokpenda zaidi, kuna wanaopenda keki za chocolate zaidi na wanaopenda keki za nazi zaidi.
Ladha ya keki ndo kitu ambacho kinanogesha zaidi, utamu wa keki sio tu sukari bali ni ile ladha inayopatikana. Mapambo pia yanachangia zaidi kwenye kuleta mteja au kumuondoa mteja wa keki.
Mpambaji wa keki unatakiwa uwe mbunifu kulingana a aina ya tukio na muhusika wa tukio. ndio maana kekik za watoto wadogo zina mampambo tofauti na keki za watu wakubwa, Vilevile keki za mtoto wa kiume zina mapambo tofaut na keki za watoto wakike. Ubunifu huu unasiaidia sana kunogesha tukio na kutofautisha aina za keki.
Ni vizuri kujua ni aina gani ya mapambo utayoenda kutumia kabla ya zoezi la kupamba keki halijaanza.
Huku kutakufanya uwe huru kuandaa mazingira ya mapambo yako, na vifaa vyote vinavyohusika katika hayo mapambo utayochagua.
Kikubwa cha kuzingatia ni mapambo ya keki na ladha ya keki.
keki iwe na muonekano mzuri kwanza ili kuvutia watu, kisha iwe na ladha nzuri ila kufanya watu watake kuendelea kula keki. Keki inahitaj maandalizi.
Je, ni vifaa gani muhimu wakati wa kupika keki?
Je, ni vitu gani vya kuzingatia katika upishi wa keki?
Je, ni zipi hatua sahihi za upishi wa keki?
Yote haya utajifunza nami katika blogu yangu.
Usisite kutoa maoni yako.
Comments
Post a Comment