VIFAA MUHIMU KWENYE UPISHI WA KEKI
Je unatamani kujifunza kupika keki lakini hujui wapi kwa kuanzia? Ungana nami kwenye mfululizo wa darasa za keki mbalimbali kwenye blog hii.
Watu wengi wanapenda sana kujifunza kupika keki. Hii ni kwasababu keki ni chakula kitamu na kizuri kwa mtu kula wakati wowote. Ni furaha zaidi kula chakula ulichopka kwa mikono yako badala ya kununua.
Ni ngumu kutaka kujifunza kupika keki bila kujua unaanzia wap. Mara nyingi kujua vifaa gani muhimu kwenye upishi ndo hua changamoto ya kwanza kukutana nayo.
Ni vipi vifaa muhimu kwenye upishi wa keki?
Kuna aina tofauti tofauti vya kupikia keki ikiwemo vinavyotumia umeme na visivyotumia umeme. Leo tutaangalia vifaa vya aina zote hizi mbili.Vifaa visivyotumia umeme
1. Mchapo
Hiki ni kifaa kwa ajili ya kukorogoea mchanganyiko wako.
Badala ya mchapo unaweza kutumia mwiko kukorogea kama wengi wetu tulivyozoea.
2. Mzani
Huu ni mzania mdogo kwa ajili ya matumizi ya jikoni. Mara nying mizani hii hutumia betri za kawaida.
Ili keki yako iive vizuri, bas unahitaji mzani kwa ajili ya vipimo sahihi ya mahitaj ya keki.
Kwenye keki kuzidi au kupungua kwa mahitaji yako kunaweza kubadilisha keki nzima hasa kwenye uivaji na uchambukaji.
unaweza usiwe na mzani nyumbai lakin ni vizuri kujua vipimo halisi vya mahitaji yako, kama vile kiasi cha unga, sukari na blueband.
3. Jiko
Hapa linaweza kua jiko la mkaa au gesi.
Unaweza soma hapa upishi wa keki kwa jiko.
4. Bakuli / Kontena
Hii ni kwa ajili ya kuchaganya mahitaji yako ya keki. Hakikisha bakuli inakua safi na kavu.
Pia chagua ukubwa wa bakuli kulingana na wingi wa mahitaji yako ya keki, ili kusaidia uchanganye vizuri bila kumwagika.
Vifaa vya vinavyootumia umeme
1. Mixer
Kuna aina tofauti za mixer. Kuna mixer kubwa na mixer ndogo.
Kwenye kjuchagua mixer inategemea na mahitaji yako mengine kama vile kukandia unga wa vitafunwa vingine na bajeti yako. Mixer kubwa zina bei kubwa kuliko mixer ndogo.
Kwenye keki unaweza ukatumia mixer ndogo ya mkono (handmixer) na ukapata keki nzuri.
Hii inatumika kuuchanganya mchanyiko wako wa keki.
2. Oven
Hili ni jiko maalumu kwa ajili ya kuoka keki. Mbali na matumizi ya keki, oven pia inatumika katika kuoka vyakula vingnine tofaut kama vile nyama, mikate na kadhalika.
Unapotumia oven ni vizuri kujua aina ya oven yako na moto wake. Hii itakusaidia wakat wa kusawazisha moto na muda wa keki yako kuiva.
Moto ukiwa mkali sana keki unaweza hatarisha keki yako kuiva na kuchambuka vizuri.
Kutokana na gharama za oveni, wengi wanatumia jiko la mkaa kupika keki.
Hivyo bas unaweza ukapika keki nzuri kwa ajili ya nyumbani na biashara bila ya oven.
Comments
Post a Comment