Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua keki

Kwenye shuguli mambo mengi hua yanatokea kuhusuiana na keki. Miongoni mwa hayo mambo ni;

  • keki kua ndogo, watu kua wengi.
  • Muonekano wa keki kutoendana na tukio husika.
  • Muonekano wa keki kutoendana na muhusika wa tukio.
  • Kununua keki kwa gharama kubwa zaidi kuliko ulivyotarajia

Ulishawahi kukutana na changamoto zipi wakati wa kununua keki?

Makosa yanaweza kua ya muuza keki au wewe mnunuaji. Sasa jifunze mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua keki ya shughuli yako.

  • Muonekano

Jambo la kwanza kabisa la kuzingatia ni muonekano wa keki unayohitaji.
Kuna picha nyingi sana za keki mitandaoni, chagua keki unahohitaji. Au wasiliana na muuza keki akutumie sampo za keki ambazo yeye anatengeneza.
Hii itakuasadia zaidi kufanya maamuz mapema katika kuandaa muonekano wa tukio na muhusika , ili rangi za keki ziendane na mapambo au nguo za muhusika.
  • Gharama
Haijalishi ukubwa wa tukio, ni vzuri kua na bajeti yako ya tukio zima mapema. 
huku kutafanya shughuli iwe na kiwango kilekile kwa gharama ile ile uliyoipanga hapo awali.
Bajeti ni kitu muhimu sana cha kukizingatia sio tu katika keki bali katika manunuzi yetu mengi ya kila siku.

  • Aina ya tukio
Ni vizuri kununua keki inayoenda na tukio. keki ya harusi inapendeza zaidi ikiwa na muonekano wa tofauti na keki za birthday. Ndio maana ni mhuimu kujua gharama ya keki unayohitaji kwa tukio husika. kama ni keki ya harusi ni lazima bajeti yake iwe kubwa zaidi tofaut na keki za matukio mengine. Ni muhimu kutofautisha aina ya tukio.
  • Ladha
Kuna keki zenye ladha tofauti. Mtu hua anafurahia keki yenye ladha ile ambayo hua anapendelea. Ladha hyo inaweza kua, ladha ya chocolate, vanilla au chungwa, na kadhalika
Ni muhimu kumwambia muuza keki ni ladha ipi unayohitaji kwenye shughuli yako. Vile vile anaweza kukushauri ni aina gani gani ya keki ambayo watu wanaipenda kulingana na tukio husika. kuna aina ngapi za keki? bonyeza hapa.
  • Chagua mpishi wako
Wnaopika keki ni wnegi sana. Na wote hao wanatofautiana kwenye mapishi, gharama na maeneo. Kuchagua mpish wako mapema  kutakufanya uwe na machaguzi mazuri kwenye bajeti, hii kuanzia kwenye mapish ya hiyo keki had kwenye usafir kukufikia ulipo. Usipojua keki utaenda kununua kwa nani mapema kutakuafnay uchelewe na utajikua unaenda kununua keki popote pale. Hii inachangia kuvuruga bajeti yako na kupata keki ambayo haijaendana sana na tukio. Na ndiomana Datie's Cakes tunashauri uweke oda mapema upate kile unachokitaka kweny shughul yako.


Hayo ni baadhi tu ya mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa kununua keki kwa ajili ya party yako.
Tunafurahia shughuli zetu kwa keki, ili ufurahie vizuri ni lazima kula keki yenye kiwango kizuri, muonekano mzuri, ladha nzuri ndani ya bajet yako. 

Comments

Popular Posts