UPISHI WA KEKI KWENYE JIKO LA MKAA
Kumekua na maswali mengi juu ya upishi wa keki kwa kutumia jiko la mkaa.
Kuna changamoto nyingi sana kwenye upishi wa keki kwa kutumia jiko hili.
Ila ukiliwezea, kila kitu kitakua sawa na utafurahia upishi wako.
CHANGAMOTO ZA UPISHI WA KEKI KWA JIKO LA MKAA
Changamoto zipo tofauti tofauti, kwenye upishi wa keki kiujumla.
Lakini changamoto zinazotokana na jiko la mkaa mara nyingi ni
- keki kutoiva vizuri
- kuungua sana juu au chini
- keki kunywea na kua na bonde
- keki kupasuka sana
- keki kuiva kama ugali.
Changamoto hiz mara nyingi husababishwa na moto.
Moto ukipungua sana keki lazima iwe na kasoro na moto ukizidi lazima kuwe na kasoro pia.
Hivyo basi, upishi wa keki kwenye jiko la mkaa unahitaji umakini zaidi kwenye kukadiria moto wa chini na wa juu.
NAMNA YA KUPIKA KEKI KWA JIKO LA MKAA.
- Baada ya kuchanganya mchanganyiko wako vizuri kabisa. sasa ni wakati wa kuuweka kweny moto wa jiko la mkaa.
- Hakikisha moto wako umekolea vizuri
- Mkaa wako usiwe wa kufubaa au kujizima wenyewe.
- Baada ya moto wako kukolea vizuri chukua sufuria kubwa ambayo itaruhusu chombo cha kupikia keki kuingia na kuenea.
- Hakikisha unaweka kitu chochote ndani yake,. hapa unaweza weka mchanga au lkibat kitachozuia chombo ha kupikia keki kugusana na sufuria kubwa.
- Weka jikon sufuria kubwa kwa muda wa dakika 4 had 5 ukiwa umefunika.
- Baada ya hapo weka chombo chako cha kupikia kikiwa na mchanngyiko wako ndani ya sufuria kubwa uloiweka jikoni. Weka moto juu mwing kias inategeme na mchnanganyiko wako uko umbali kias gani kutokoea kwenye mfuniko wa sufuria.
- Weka na moto chini pia kiasi. jitahidi usiwe mwingi sana keki yako itaungua na wala usiwe mdogo sana keki yako ita nywea na kutoka kama ugali.
Kwenye upishi wa keki, jizuie kufunua keki yako mara kwa mara baada ya kuiweka kwenye moto. Huku kunasababisha mchanganyiko ubonyee na kusababisha bonde kwenye keki.
Kuangalia keki yako kama imeivaa ni dakika ya 45 na kuendelea baada ya kuiweka kwenye moto sahihi.
Comments
Post a Comment